
Mjasiri haachi asili na akiacha asili si jasiri tena hiyo imedhihirika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baada ya staa aliyekuwa anasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka Tanzania, Wayne Rooney kuchungulia nyavu za miamba wa Kenya, Gor Mahia kuandikia goli la kuongoza kwa timu yake mpya ya Everton dakika ya 34 kipindi cha kwanza.

Unashuhudia staa huyo akiendelea kukimbiza katika kikosi hicho na kuonyesha ubora wake na kuandika historia ya kufunga katika ardhi ya Tanzania, ikiwa pia ni bao lake la kwanza kwenye mechi ya kwanza tangu ajiunge na Everton msimu huu akitokea Manchester United.

Katika kipindi cha kwanza Rooney alipachika goli hilo kwa umahiri na kuwainua mashabiki wake lakini baada ya dakika mbili baadaye, Gor Mahia walisawazisha kupitia kwa Tuyisenge mabao yaliyodumu kwa kipindi chote cha kwanza.
Kipindi cha pili Everton walionekana kuumudu mchezo ipasavyo huku Dowel akiipatia Ecerton bao la kuongozadakika ya 82, bao lililodumu mpaka kipyenga cha mwisho ambapo matokeo yalikuwa Everton 2-1 Gor Mahia.
PICHA: RICHARD BUKOS NA MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS