×

Waziri Ashutumu Fedha za Ujenzi Madarasa Kuhamishwa

Stella Manyanya aliyetangulia akikagua majengo ya shule hiyo.

 

NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya,  amelaani kitendo cha fedha zilizohamishwa kutoka Shule ya Sekondari ya Kambangwa Kinondoni Dar, na kupelekwa katika Shule ya Sekondari ya Mbweni bila utaratibu maalum wa kuzitaarifu mamlaka zinazohusika ikiwemo ofisi yake.

 

Stella Manyanya na timu yake wakikagua majengo ya madarasa yanayojengwa shuleni hapo

 

Hayo ameyaeleza wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea shule hiyo ambapo alikutana na Ofisa Takwimu wa Wilaya ya Kinondoni, Ramadhan Mabara aliyemweleza kuwa fedha za ujenzi wa mabweni mawili, madarasa manne ambayo yakimalizika yatachukua wanafunzi wa kidato cha tano na sita na vyoo.

 

Wanafunzi wakimsikiliza Stella Manyanya darasani (hayupo pichani).

 

Manyanya alisema amefurahishwa na utendaji wa kazi unaoendelea shuleni hapo japokuwa hakukubaliana na uhamisho wa fedha zilizotoka Kambangwa kwenda shule hiyo nje ya utaratibu wa kiserikali.

 

Stella Manyanya akiwaasa wanafunzi hao.

 

Aidha alipata fursa ya kuzungungumza na baadhi ya wanafunzi na akawaasa wasome kwa bidii ili wafikie malengo na serikali itaendelea kuongeza baadhi ya vifaa vya maabara kulingana na uhitaji ili wanafunzi waweze kukidhi viwango vya elimu.

 

Ujenzi ukiendela.

 

NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave a Comment