
WAKATI harakati za usajili zikizidi kupamba moto, Ndanda FC ya mkoani Mtwara ipo katika hatua za mwisho za kumalizana na aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu.
Ndanda inataka kumsajili Busungu kwa ajili ya kuiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji kwa ajili ya kuhakikisha inakuwa moto wa kuotea mbali msimu ujao.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya Ndanda, zimedai kuwa timu hiyo imemuandalia Busungu mkataba wa mwaka mmoja na muda wowote kuanzia sasa atamwaga wino wa kuitumikia.
STORI: SWEETBERT LUKONGE | CHAMPIONI JUMAMOSI