×

Kagera Sugar Wampotezea Bokungu

Beki wa zamani wa Simba raia wa DRC Congo, Janvier Bokungu (kushoto) akifanya yake na Haruna Niyonzima.

TIMU ya soka ya Kagera Sugar tayari imefunga zoezi la usajili wake wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara unaotarajia kuanza Agosti 26, mwaka huu.

Kutokana na hali hiyo, beki wa zamani wa Simba raia wa DRC Congo, Janvier Bokungu hatoweza tena kujiunga na Kagera Sugar ambayo Bokungu alikuwa anatamani kuitumikia msimu ujao.

Meneja wa Kagera Sugar, Mohammed Hussein ameliambia Championi Jumamosi kuwa, nafasi za kusajili walizobakiza ni nne tu na wamepanga kuzijaza katika dirisha dogo la usajili.

STORI: SWEETBERT LUKONGE | CHAMPIONI JUMAMOSI

Tazama Maajabu ya Maji Kupandisha Mlima Eneo la Kijungu- Rungwe

Leave a Comment