
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo September 9, 2017 imeutaka upande wa mashtaka katika upelelezi wa kesi inayomkabili Rais wa Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kuwa wakweli.
Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa alisema hayo baada ya Wakili wa Serikali, Nassor Katuga kudai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba bado nyaraka hazijawa tayari kutoka kwa mtaalamu wa maaandishi.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa aliutaka upande wa mashtaka kuwa wakweli na kuhakikisha upelelezi unakamilika haraka. Aidha Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba18, mwaka huu.
NA DENIS MTIMA | GPL