×

Madenti Mashindano ‘Genius Cup’ Watunukiwa Vyeti

WANAFUNZI
Mkurugenzi wa Shule za Sekondari za Feza, Ibrahim Yunus akikabidhi cheti kwa mwanafunzi
WANAFUNZI
Wanafunzi watatu waliofanya vizuri zaidi katika masomo ya Hisabati waliotunukiwa kiasi cha fedha 200,000 kwa mshindi wa kwanza (150,000) mshindi wa pili na laki moja kwa mshindi wa tatu.
WANAFUNZI
Mkurugenzi Yunus na Mwalimu wa wanafunzi hao, wakiwa katika picha ya pamoja na washindi sita wa masomo ya Hisabati.
WANAFUNZI
Mkurugenzi Yunus akiendelea kukabishi vyeti kwa wanafunzi walioshinda mashindano hayo
WANAFUNZI
Mkurugenzi Yunus akiendelea kukabishi vyeti kwa wanafunzi walioshinda mashindano hayo
WANAFUNZI
Taswira ndani ya ukumbi wa Sekondari wa Feza wakati wa hafla hiyo.

WANAFUNZI 60 kutoka katika Shule za Sekondari za Feza jijini Dar es Salaam, jana walitunukiwa vyeti vya ushindi baada ya kufanya vizuri katika masomo ya sayansi, wakishindana na wanafunzi wenzao wapatao 3000 kutoka mikoa kumi nchini.

 

Katika hafla ya kukabidhi vyeti hivyo, iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Kimataifa ya Feza, Salasala jijini Dar, Mkurugenzi wa shule hiyo, Ibrahim Yunus alisema mashindano hayo ya kimasomo yajulikanayo kama Genius Cup, yaliandaliwa kwa pamoja na shule hizo kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Commission of Science and Technology.

 

“Lengo letu ni kuwaandaa wanafunzi ili watakapomaliza masomo yao wawe na taaluma ya kisayansi, hasa kwa kuwa nchi inaelekea katika uchumi wa viwanda, hivyo inahitaji vijana wanasayansi na mashindano haya hufanyika kila mwaka hapa nchini,” alisema mkurugenzi huyo na kuitaja baadhi ya mikoa iliyoshiriki kuwa ni Tanga, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Mtwara, Pwani, Arusha na Zanzibar.

 

Mbali na kupewa vyeti, wanafunzi watatu waliofanya vizuri zaidi katika masomo ya Hisabati walitunukiwa kiasi cha fedha 200,000 kwa mshindi wa kwanza (150,000) mshindi wa pili na laki moja kwa mshindi wa tatu.

Leave a Comment