The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi Barani Afrika Wakutanishwa Dar

1
Mkurungenzi wa Shule zote za Al Muntazir Islamic Seminary, Mahmood Ladak akizungumza na wanahabari leo.

WANAFUNZI wapataao 250 kutoka katika shule mbalimbali Barani Afrika wamejitokeza kushiriki katika mashindano ya mdahalo ulioanza leo katika Shule ya Al Muntazir Islamic Seminary, iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwajengea wanafunzi hao uzoefu wa kijieleza, kujiamini na kuweza kufanya vizuri katika soko la ajira.

 

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurungenzi wa Shule zote za Al Muntazir Islamic Seminary, Mahmood Ladak, amesema mashindano hayo yameshirikisha shule 15 kutoka Tanzania na nyingine kutoka nchi kama Zimbambwe, Afika Kusini na Uganda.

 

Amesema lengo la mashindano hayo ni kuwakutanisha wanafunzi hao wa kutoka shule nyingine ili kujadiliana mawazo mbalimbali ya kielimu waliojifunza darasani.

 

 

Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na Mwl. Nyerere School Inventation Debate Championship yanayotarajiwa kumalizika Agosti13 mwaka huu. katika mjadala huo kuna mada mbalimbali ambazo wanajadili ikiwemo national system na kuhusu Sudan Kusini kujiunga katika nchi za Afrika Mashariki EAC.

 

Kwa upande wake, Mratibu wa Taasisi inayohusika na mjadala, Dominic Mwakifulele amesema katika kuandaa mdahalo huu walitumia utaratibu wa kujiandikisha (process registration), kutumia mitando ya kijamii kwa lengo la kuhamasisha ushiriki wa shule.

 

Naye mwanafunzi, Hawa kutoka katika shule ya Al Muntazir ya hapa nchini ameshukuru uongozi wa shule hiyo kuandaa mashindano kama hayo kwani yatawajenga kielimu katika masomo yao.

1 Comment
  1. […] yote hayo ni ya watu wenye asili ya Afrika, kwa kuwa walikuwa weusi tii! Leo nakuletea Wahindi Wekundu wa Kabila la Huarorani, hawa wanaishi […]

Leave A Reply