×

Nduda: Nikipona Tu Manula Anatoka Golini

Kipa wa Simba, Said Mohamed.

SAID Mohamed ‘Nduda’ ni kipa wa Simba am­baye amesajiliwa msimu huu aki­tokea Mtibwa Sugar ya mko­ani Morogoro a m b a p o hadi sasa hajaichezea mechi hata moja ka­tika Ligi Kuu Bara kwa msimu huu wa 2017/18, sababu kubwa ni kutokana na kuwa majeruhi.

Nduda ambaye ndiye kipa bora wa michuano ya Cosafa iliyofanyika nchini Afrika Kusini hivi karibuni, alianza kuugua goti tangu al­ipokuwa katika maandalizi ya msimu huu wakati timu yake ikijiandaa kucheza dhidi ya Yanga ka­tika Ngao ya Jamii wakati huo Simba ilikuwa visiwani Zanzibar.

Tangu hapo amekuwa nje ya uwanja hadi hivi sasa huku ikielezwa kuwa anajiandaa kwa sa­fari ya kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

Safari yake hiyo imekuwa ikipigwa danadana kila kukicha. Gazeti la Championi Ijumaa limeku­tana na kipa huyo wa zamani wa Yanga, na hapa anafunguka.

UNAZUNGUMZIAJE MAJERAHA YAKO?

“Nimekuwa katika wakati mgumu wa kuona goti lilianza muda mrefu tangu nilipokuwa na timu ya Mtibwa Sugar msimu uli­opita ambapo lilikuwa likinisumbua japokuwa nilipatiwa matibabu.

“Baada ya matibabu niliendelea kuwa fiti na kufanya kazi zangu kama kawaida na hata ka­tika mashindano ya Cosafa yaliyofanyika nchini Afrika Kusini hivi karibuni nilipokuwa timu ya taifa, tatizo hili halikujitokeza.

“Goti lilianza kunisumbua tena wakati na­jiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga iliyochezwa Agosti 23, imekua hivyo hadi sasa.

VIPI KUHUSU SAFARI YA INDIA?

“Upande wangu nausubiri uongozi ambao ndiyo umepanga safari hiyo na pindi itakapokamilika m i m i n i ­takuwa t a y a r i k w e n d a , awali kitu kilichokuwa kikik­wamisha ilikuwa ‘visa’ lakini kwa sasa tayari nimeshaipata ila sijajua nini kinaendelea na mimi nawasiki­liza wao ndiyo wenye maamuzi ya mwisho.

KWA SASA UNAFANYA SHUGHULI GANI?

“Natumia muda mwingi kujipumzisha ili kujiweka sawa kimwili na kiakili kwa sababu hivi sasa naendelea na matibabu tu ya hapahapa huku nikisubiri safari. Sina shughuli nyingine yoyote ninayoi­fanya nje ya mpira zaidi ya kusikilizia afya yangu.

UNAZUNGUMZIAJE KUKAA NJE MUDA MREFU?

“Ni kweli niliambiwa kuwa pindi nitaka­porejea nitakaa nje ndani ya wiki nne hadi sita bila ya kufanya shughuli yoyote ya kimpira, kwa upande wangu sijisikii vizuri, lakini naamini nitakapopata nafuu nitarudi katika hali yangu.

UNADHANI MAJERUHI YATAKUPOTEZEA NAMBA?

“Ushindani wa namba ndani ya Simba upo mkubwa sana na hasa ukizingatia kila mchezaji anahitaji kucheza, kikosi chetu ni kipana kwa sasa, lakini mwisho wa siku mwalimu ndiyo mtu wa mwisho kufanya maamuzi ampange nani.

“Kwa upande wangu sina tatizo lolote juu ya uwepo wa (Aishi) Manula ila najua nikipona nitapata nafasi ya kucheza, kikubwa zaidi ni kujituma katika mazoezi ili kuendelea kuwa fiti kwani ninauamini uwezo wangu.

NENO LAKO KWA SIMBA KATIKA MBIO ZA UBINGWA MSIMU HUU?

“Kuzungumzia suala la ub­ingwa kwa sasa ni mapema mno japokuwa moja ya malen­go yetu ni kuona tunafanikiwa kuwa mabingwa msimu huu, hasa ukizingatia usajili uliofan­ywa msimu huu ni mzuri.

“Kitu cha msingi ni kuona tu­nafanikiwa kushinda katika kila mchezo ili iweze kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi, kila mchezaji angependa kuona tunafanikiwa mwisho wa msimu.

UNAZUNGUMZIAJE UWEPO WA OKWI, NIYONZIMA NDANI YA SIMBA?

“Wachezaji hawa ni maprofesh­eno hivyo uwepo wao kikosini kuna umuhimu wa hali ya juu na watatoa msaada mkubwa kuhakikisha wanaisaidia timu kufika kule ambapo imetarajia kufika.

“Mfano mzuri tunawe­za kuona jinsi Okwi anavyoifungia timu kwa sasa ambapo hadi sasa ana mabao sita, hivyo ni mwan­zo mzuri.”

SIRI Imefichuka Baada ya Kushushwa kwa Bilionea Yanga wa Kulipa Mishahara

Leave a Comment