
Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC (“Vodacom”) leo imetangaza matokeo ya hesabu zake kwa kipindi cha nusu ya mwaka ulioishia Septemba 30, 2017.
Matokeo hayo yanaonyesha kuimarika kwa biashara pamoja na ukuaji wa mapato ya huduma, ambayo yalisababishwa na ukuwaji wa huduma M-Pesa na pamoja na data. Mapato yatokanayo na huduma pia yamekuwa huku mtiririko wa fedha ukikua kwa asilimia 73.2 hadi kufikia shilingi bilioni 58.3 kwenye kipindi hicho.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom’s, Bw. Ian Ferrao alisema , “Mwaka 2017 umekuwa ni mwaka muhimu kwa Vodacom Tanzania. Kwa miezi ya hivi karibuni, zoezi la uuzaji wa hisa limekamilisha mauzo ya toleo la awali la (IPO), ambalo lilikuwa ni kubwa zaidi katika historia ya soko la hisa la Dar es salaam (DSE),
Tume fanya mkutano wetu mkuu wa kwanza wa mwaka, tukiwa kama kampuni ya umma. Tumetangaza gawio la kwanza kama kampuni iliyoorodheshwa DSE na kutokana na mikakati tuliyojiwekea tumepata matokeo chanya yaliyochagizwa na kasi ya kibiashara,ukuaji thabiti wa mapato yatokanayo na data,M-pesa,na huduma kwa taasisi mbalimbali,”
Ferrao aliongeza “biashara yetu imeleta matokeo chanya kutokana na uwezo wa kibiashara na ukuaji wa mapato kwa upande wa data, M-Pesa na huduma nyingine”.
Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa, matokeo hayo chanya yaliyopatikana ndaniya muda mfupi yanatia moyo na kuonyesha kuwa huduma zinazotolewa na kampuni hiyo ni bora na zinakubalika zaidi
Alisema M-Pesa na huduma nyingne zinazozingatia matakwa ya wateja,vilisaidia kukuza biashara katika kipindi kilichgo ushindani mkubwa wa soko.
“Pamoja na changamoto za kibiashara nchini Tanzania, mapato yetu yameendelea kuimarika, kukuza idadi ya wateja, kuendelea kushikilia nafasi yetu kama kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za simu za mkononi na za kifedha,” alisema
Mkurugenzi huyo aliafanua kuwa, mafanikio yaliyopatikana ni matokeo ya kuendelea kwa uwekezaji uliohitajika na ambao umefanyika katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Alisema, uwekezaji huo umewezesha na kusaidia ongezeko la wigo wa huduma na kuiweka kampuni kwenye nafasi ya mbele kwa upande wa huduma za kifedha na data.
Katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka huu wa fedha, Vodacom imewekeza kiasi cha shilingi bilioni TZS 102.4 bn katika kupanua wigo wa kuongeza mtandao.
“Uwekezaji huu ulilenga zaidi kuongeza uwezo wa mtandao. Tuliongeza uwezo wa huduma ya data ya 3G kwenye minara yetu iliyopo kwenye miji mikubwa kwa zaidi ya asilimia 25, wakati huo huo tukizindua huduma ya 4G kwenye majiji matatu, na kuboresha huduma hiyo kwenye jiji la Dar es Salaam.
Kwa kushirikiana na wabia wetu, kampeni ya kuwezesha upatikanaji wa simu za gharama nafuuKampeni mkononi za kisasa “Smartphone” ilifanikiwa sana, kwani ushahidi umeonyesha idadi ya wateja imekuwa hadi kufikia asilimia 27 ya soko la simu .
Tunapoingia katika nusu ya pili ya mwaka wetu wa fedha, tunaendelea kukuza huduma na matumizi ya data ikiwemo kwa simu zisizo Smartphones na kuwalenga wateja wanaotumia kiwango kidogo cha data. Kwa kupitia lengo letu la kuongeza wigo wa huduma, tutaendelea kuwa kwenye nafasi ya kwanza dhidi ya washindani wetu kutokana na kutilia mkazo ubora wa mtandao na huduma kwa wateja,” alisema Ferrao.