×

Mtandao wa Muziki Nchini Wampongeza Kampuni Ya Msama Auction Mart

Mkurugenzi Mtendaji wa Msama Auction Mart, Alex Msama (kulia) akizungumza na waandishi wa habari baada ya oparesheni kumalizika.
Msama akiwa amebeba Kopyuta zinazotumika kudurufu CD feki baada ya kuzikamata.

 

MTANDAO  wa Muziki Tanzania (TAMUNET) umempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Msama Auction Mart kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiendelea nayo  ya kukamata wezi wa kazi za muziki na hivyo kutoa mchango mkubwa katika kupunguza uharamia na kuhamasisha uchangiaji wa pato la Taifa.

 

Katika pongezi hizo Mwenye kiti wa Tanzania Musicians Network , John Kitime alisema kuwa kwa niaba ya wanachama wa Tanzania Musicians Network kwamba wanaomba kutoa  shukrani za dhati kwa mchango wake mkubwa ambao kampuni yake inaufanya katika jitihada za kupunguza uharamia wa kazi za wasanii.

 

‘Tuko tayari kushirikiana nawe kila wakati kwa lengo la kuboresha mazingira yanayohusu uboreshwaji wa stahiki za wanamuziki wakati wowote, hasa lengo kubwa hata serikali iweze kupata kodi stahiki,” alisema.

 

Msama aliendelea kueleza kuwa hataweza kuvunjwa moya na baadhi ya vikundi vya watu wachache wanaopinga zoezi hilo la ukamataji kazi za wasanii katika jiji la Dar es Salaam.

 

‘Tumetembelea maeneo ya Manzese, Mwenge na maeneo ya Tegeta na tumewakamata wanaodurufu CD feki na kuikosesha serikali mapato. Tutaendelea kupambana na wezi wa kazi za wasanii tukishirikiana na jeshi la polisi popote pale iwe usiku au ufichoni

tutawafikia,” alisema msama baada ya kumalizika kwa opareshe maeneo hayo.

 

 

Leave a Comment