×

Serengeti Boys Wafanya Mazoezi Uwanja wa Hoteli ya The Xanthe, Uturuki


KIKOSI cha timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Boys inayoshiriki mashindano ya Uefa Assist nchini Uturuni, leo wamefanya mazoezi mepesi katika uwanja wa Hoteli ya Xanthe ili kujiweka sawa kwa ajili ya mechi zijazo katika kundi lake.

Mazoezi hayo yanafuatia mechi yao ya jana dhidi ya Guinea waliyoianza kwa kufungwa kwa bao 1-0.

Katika mazoezi ya leo, Serengeti Boys walikimbia mitaani sehemu mbalimbali hapa jijini Antalya na baadaye kurejea kwenye Uwanja wa Tenisi katika hoteli ya The Xanthe walipofikia na kufanya mazoezi mepesi zaidi.


Kesho watashuka dimbani kucheza na wenyeji Uturuki katika michuano hiyo ambayo haina bingwa.

Michuano hiyo ni kwa ajili ya kujiweka sawa kwa michuano mbalimbali na hakuna bingwa wala mshindi wa pili.

Na Saleh Ally, Antalya