Wakati mazoezi ya kikosi cha Simba yamemalizika mashabiki wa Simba walionekana kuwa na hamu ya kuzungumza kuelekea mchezo huo huku Global TV Online ikihakikisha inawapa fursa ya kutoa maoni yao kuelekea mchezo huo.
Baadhi ya Mashabiki wametoa utabiri wao kuelekea mchezo huo ambapo wamesema watafunga magoli 3-0 hatua ya Robo Fainali Ligi ya mabingwa Barani Afrika utakaopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.