×

Mbowe, Nyalandu, Mnyika, Lema, Sumaye Wahudhuria Uhuru Day – Video

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu,  wamehudhuria sherehe za kutimiza miaka 58 tangu Tanganyika (Tanzania Bara) ipate uhuru ambazo zinafanyika jijini Mwanza kitaifa katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo. 

Taarifa ya kushiriki kwenye maadhimisho kwa Mbowe ilitolewa juzi na kamati kuu ya chama hicho kwa kumwagiza akiwakilishe chama hicho kwenye sherehe hizo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Chadema kushiriki maadhimisho ya uhuru tangu mwaka 2015.

 

Viongozi wengine waliohudhuria ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani kabla ya kukihama chama hicho hivi karibuni na ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, aliyeungana na mawaziri wakuu wastaafu wengine ambao ni Edward Lowassa na Mizengo Pinda.

 

Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini, wamehudhuria maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Mwanza.

LIVE: RAIS MAGUFULI ANAHUTUBIA MIAKA 58 YA UHURU MUDA HUU

Leave a Comment