
MWIGIZAJI Yusuf Mlela ametamba kuupa kisogo umaskini kwa kuwa ndani ya miezi michache, maisha yake yamebadilika kinoma na kuwa bomba, tofauti na zamani kwani alishakata tamaa kwenye uigizaji.
Mlela ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, ndoto yake ya kumiliki gari au kula msosi mzuri ilishafutika, lakini sasa Mungu amemuona.
“Siku zote Mungu hamtupi mja wake. Kuna muda ulifika nikajua ndoto yangu ya kumiliki gari aina ya Toyota Harrier imefutika, lakini sasa Mungu ameniona,” amesema Mlela ambaye juzikati alizuliwa timbwili na aliyekuwa mpenzi wake, Annastazia Exavery ‘Ebitoke’.
Stori: Imelda Mtema, Dar