
Wasanii wa muziki wa Bongo Flava, Harmonize na Kusah, wameungana na kutoa wimbo mpya wa mapenzi uitwao “Kama Sio.” Wimbo huu unachanganya sauti za kipekee, mashairi yenye hisia kali, na melodi laini za Bongo Flava, ukielezea upendo wa dhati na uaminifu katika mahusiano.
Kusah na Harmonize wanachukua nafasi kubwa ya kuonyesha ustadi wao katika muziki wa kizazi kipya.
“Kama Sio” ni wimbo unaovutia sana na kugusa mioyo ya wapenzi wa muziki wa Bongo Flava, huku Kusah na Harmonize wakionyesha umakini katika kutunga na kutekeleza kazi yao ya kipevu. Sauti zao, kwa pamoja, zinautamu wa pekee, na zitafanya mashabiki kuendelea kuusikiliza wimbo huu kwa muda mrefu.

Kilichovutia mashabiki zaidi ni Video vixens waliotumika katika video ya wimbo huu. Kwa upande wa Harmonize, amemtumia mpenzi wake Kajala katika video hiyo, na Kusah alijibu kwa kumtumia mpenzi wake, Aunt Ezekiel. Hii imeongeza mvuto na kupamba zaidi video, ambapo mashabiki walivutiwa na uhusiano wa wapenzi hawa wawili wakifanya kazi pamoja na kuonyesha upendo wa dhati.
Harmonize na Kusah wamefanikisha kutengeneza wimbo ambao unawavutia watu wengi, na video yake ni kivutio cha ziada kwa wapenzi wa muziki na mashabiki wa sanaa.