
WATU wapatao 24 wamepoteza maisha na wengine 16 kujeruhiwa jana nchini Indonesia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupoteza mwelekeo na kuanguka katika korongo.
Mkuu wa kituo cha habari cha shirika la usimamizi wa janga la mkoa huo, Nopriyaddin, amesema leo kuwa ajali hiyo ilitokea katika mkoa wa Sumatra kusini mwa nchi hiyo.
Waliojeruhiwa walikimbizwa kwenye hospitali ya karibu kupata matibabu na kwa mujibu wa Nopriyaddin, idadi ya waliofarika inaweza kuongezeka kwani abiria wengi walijeruhiwa vibaya.