
MME na mke waliokuwa wakisafiri kwenda kula sikukuu ya Krismas wamefariki katika ajali katika daraja la Mwiwondwe barabara ya Ekero-Buyangu nchini Kenya. baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupoteza mwelekeo na kuanguka.
Wanandoa hao waliofariki alfajiri ya jana walikuwa safarini kuelekea Busia kwa ajili ya sherehe za mwisho wa mwaka (Krismasi na Mwaka Mpya).
Miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Mtakatifu Maria wa Mumias. Polisi imetoa tahadhari kwa watu wanaotumia vyombo vya moto wawe waangalifu.