
MEDDIE Kagere mshambuliaji wa Simba guu lake juzi limeibuka Uwanja wa Uhuru baada ya kupita dakika 229 alizocheza bila kuzifumania nyavu.
Kagere ambaye amefunga mabao tisa mpaka sasa kwenye ligi, mabao matano amefunga kwa guu la kulia huku mawili akifunga kwa guu la kushoto na mawili kwa kichwa, mara ya mwisho kufunga ilikuwa mbele ya Mbeya City wakati Simba ikishinda mabao 4-0 Uwanja wa Uhuru.
Mshambuliaji huyo Mrwanda, alicheza dakika 229 bila kufunga bao mbele ya Tanzania Prisons mchezo ulioisha suluhu kisha ule dhidi ya Ruvu Shooting Simba walishinda mabao 3-0 yeye hakufunga mpaka alipoifunga Lipuli dakika ya 49 na kufanya zitimie dakika 229 bila kufunga pale Uhuru.
Katika mchezo huo dhidiya Lipuli ambao Simba walishinda mabao 4-0, Kagere alifunga bao moja akiunganisha vyema pasi aliyopewa na kiungo Clatous Chama.
Kagere ambaye msimu uliopita alifunga mabao 23 nakuwa mfungaji bora kwenye ligi kuu aliliambia Championi
Jumamosi kuwa, kila siku anajipa changamoto yeye mwenyewe ili aweze kuwa bora zaidi.
Stori na Wilbert Molandi, Dar es Salaam