
KATIKA kuongeza hamasa ya timu, uongozi wa Yanga juzi usiku umekutana na wachezaji wake na kufanya kikao kizito katika kuelekea pambano la leo litakalowakutanisha dhidi ya watani wao wa jadi Simba na kati ya hao, wapo wapya Haruna Niyonzima na Ditram Nchimbi.
Pambano hilo limepangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam linalotarajiwa kujaa upinzani mkubwa kwa kila timu kupania kupata ushindi ili kutengeneza rekodi na pointi tatu.
Viongozi hao walikutana na kuzungumza na wachezaji hao Regency Hotel iliyopo Mikocheni, Dar ambako wameweka kambi ya kujiandaa na pambano hili kubwa.

Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo, viongozi hao walikutana na kufanya kikao hicho mara baada ya mazoezi ya juzi jioni yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria, Dar kilichoendana na chakula cha jioni.
Mtoa taarifa alisema kuwa baada ya chakula hicho kumalizika, kikao kizito kilifanyika kati ya wachezaji na viongozi kilichoongozwa na Mwenyekiti wa timu hiyo, Mshindo Msolla kwa lengo la kuwajenga kisaikolojia huku wakitahadharishwa baadhi ya vitu.
Aliongeza kuwa, wachezaji walitahadharishwa kucheza kwa nidhamu kubwa kwa hofu ya kutopata kadi nyekundu huku wakipewa onyo la kutoongea na waamuzi na badala ya kucheza soka pekee katika pambano hilo huku ikitolewa ahadi ya Sh Mil 50 kama wakiwafunga Simba.
“Kama unavyofahamu mara nyingi mechi hizi za Simba, Yanga zinakuwa na upinzani mkubwa mara timu hizo zinapokutana, lakini presha kubwa inakuwa kwa wachezaji hali inayosababisha kucheza kwa kupaniki kitu ambacho ni kibaya.
STORI NA WILBERT MOLAND, GPL