×

Simba, Yanga Baada ya Dakika 90M, Hatutaki Visingizio Leo

IMEKUWA ikitokea mara nyingi katika mechi za watani wa jadi, Simba na Yanga kusikia malalamiko kutoka kwa makocha au viongozi pindi timu mojawapo inapofungwa.

 

Simba na Yanga zinakutana leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, ikiwa ni mara ya kwanza msimu huu wa mwaka 2019/20 ambao Yanga wakiwa wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 24, Simba wako kileleni wakiwa na alama 34.

Championi Jumamosi tunaamini makocha wa timu zote watakuwa wameviandaa vikosi vyao vizuri, hivyo tunatarajia kuona mechi nzuri na ya kuvutia leo na pia suala la visingizio vya kuonewa mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo hatutaskia.

Tunawaomba makocha, Sven Vandenbroeck wa Simba na Charlse Mkwasa wa Yanga kila mmoja kukubaliana na matokeo yoyote yatakayojitokeza kwa kuwa katika soka kuna matokeo matatu, kushinda, kufungwa na kutoka sare.

 

Sasa tutatashangaa kuona mkianza kurusha maneno hovyo ilhali mnatambua ninyi ni makocha wakubwa yaani wa ngazi za kimataifa. Kila la heri timu za Simba na Yanga pamoja na nyingine zote zilizobaki kwenye muendelezo wa Ligi Kuu Bara.

STORI: Bodi ya Uhariri/ Maoni

Leave a Comment