×

JPM Amuonya Mkandarasi, Ampiga Biti Katibu Mkuu – Video

 

 


RAIS John Magufuli leo Jumamosi Januari 11, 2020,  anaendelea na ziara yake ya kikazi visiwani Zanzibar ambapo ameweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwanakwerekwe iliyopo Mjini Magharibi na Hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Hotel Verde Azam Luxury Resort and Spa iliyopo Mtoni Unguja na jiwe la msingi la Jengo la Idara ya Usalama wa Taifa Zanzibar.

 

“Ni siku chache tu tumeuanza mwaka mpya wa 2020, nitumie fursa hii kuwatakia wananchi wote wa Zanzibar pamoja na Watanzania kwa ujumla, heri ya Mwaka Mpya, na mwaka huu uwe wa amani, furaha, mafanikio kwa kila mtu na nchi yetu.

 

“Elimu ndiyo ukombozi wa kila kitu, ni lazima watoto wetu wasome, wafaulu na siyo tu kuwa wasindikizaji.  Binafsi huwa naumia sana ninapoona matokeo ya mitihani, shule zinazoshika mkia ni za kutoka Zanzibar, ni lazima muweke mikakati ya kuondoa hilo.

 

 

“Hii shule ya Mwanakwerekwe ninayoweka jiwe la msingi leo, hata watoto wa Maalim Seif watakuja kusoma hapa, na hiyo ndiyo Zanzibar tunayotaka kuijenga yenye upendo na amani.

 

“Tunakopeshereheka kwa sababu sisi ni matajiri tusingekuwa na uwezo wa kulipa tusingekopeshwa, mpaka Machi jengo hili wanafunzi wawe wanaingia, hela inayotumika hapa ni ya Wanzanzibar na watailipa… Katibu Mkuu marufuku kuwatetea wakandarasi wakikupa 10% kula, ila simamia sheria.

“Haya yote ndugu zangu ni mafanikio makubwa sana. Wasione vyaelea, vyaundwa. Idadi ya watalii wanaotembelea Zanzibar imeendelea kuongezeka.

 

“Wito kwa wananchi wote wa Zanzibar pamoja na Tanzania kwa ujumla, tuendelee kushirikiana na kushikamana ili kuyaenzi, kuyalinda, kuyatetea na kuyadumisha Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964,” alisema Magufuli.

 

Leave a Comment