MVUA inayoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam imesababisha Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kufungwa baada ya kufurika na kufunikwa na maji na mvua ambayo imeanza kunyesha majira ya saa kumi za alfajiri.
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imesema mvua hizo zilizoanza kunyesha usiku wa leo katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Dar es Salaam zitaisha leo majira ya alasiri huku zikitarajiwa kunyesha tena kesho Januari 17, 2020, katika mikoa hiyohiyo.