
WATU saba wameuawa kwa mlipuko wa bomu aina ya kombora dogo (grenade) walipokuwa kwenye sherehe ya harusi huko Khartoum, Sudan.
Maofisa wa usalama na wa afya wamethibitisha tukiohilo na kuongeza kuwa watoto watatu ni miongoni mwa waliouawa.
Taarifa zinaeleza kuwa ulizuka ugomvi kati ya watu wawili na mmoja alirusha bomu hilo lililolipuka na kusababisha vifo hivyo.