×

Polisi: Wafanyabiashara wa Mabasi Hawajahujumu Reli – Video

POLISI mkoani Kilimanjaro jana Alhamisi, Januari 23, 2020, ilisema imebaini kuwa hakuna miundombinu ya reli iliyoharibiwa au kuhujumiwa katika eneo la kipande cha kutoka Moshi -Arusha.

Akizungumza nawaandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Salum Hamdun alisema:

“Niwatoe hofu wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Tanzania kwa ujumla, wananchi mtoe ushirikiano kwa jeshi la polisi juu ya taarifa kuhusiana na suala hili ikiwa ni pamoja na kuendelea kulinda miundombinu ya reli.”

 

Jumapili iliyopita, Januari 19, 2020, Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya,  aliagiza wamiliki wawili wa mabasi, Clement Mbowe mmiliki wa Machame Safari,  na Rodrick Uronu mmiliki wa Lim Safari, wakamatwe kwa tuhuma za kuunda genge la uhalifu kwa lengo la kuhujumu miundombinu ya reli ili kuathiri usafiri wa treni ya abiria kati ya Dar es Salaam na Moshi hadi Arusha.

Leave a Comment