×

Video: Mafuta Ya Mwamposa ‘Yaua’ Watu 20 Moshi, Shuhuda Asimulia

WATU 20 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa kwa kukanyagana katika harakati za kutaka kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwaiposa lililofanyika Uwanja wa Majengo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, jana jioni Jumamosi Februari Mosi, 2020.

Habari zinaeleza kuwa watu zaidi ya 40 walikanyagana katika harakati hizo za kukanyaga mafuta na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.

Idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka kwa kuwa hakuna taarifa ya ujumla ya majeruhi waliopelekwa katika vituo vya afya vya jirani pamoja na Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amelithibitishia kuwa taarifa za awali waumini 20 wamekufa lakini akasisitiza hizo ni taarifa za awali. “Taarifa za awali tulizonazo ni kuwa ni waumini 20 wamepoteza maisha lakini tunaendelea kufuatilia maeneo mengine ya zahanati, vituo vya afya na hospitali kama kuna watu walipelekwa huko,” amesema Kippi.

Taarifa zaidi zaidi za tukio hilo zinadai waumini hao walikumbwa na maafa hayo wakati wakikanyagana kwa ajili ya kugombania kukanyaga mafuta yaliyomwaga na mhubiri huyo yakidaiwa kuwa na upako.

Leave a Comment