×

Ronaldinho, Kaka Mbaroni Kwa ‘Pasipoti’ Feki


Mchezaji wa zamani wa Brazil Ronaldinho na kaka yake wamekamatwa wakituhumiwa kutumia hati bandia za kusafiria kuingia nchini Paraguay, mamlaka zimesema.

 

Polisi wa Paraguay walivamia hoteli jijini Asuncion ambako mshindi huyo wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia ya mwaka 2005 alikuwa akiishi akiwa safari yake ya kutangaza kitabu, na wakakuta nyaraka hizo za kughushi, waziri huyo alisema.

Ronaldinho na kaka yake walipokonywa hati zao za kusafiria Novemba, mwaka 2018 baada ya kushindwa kulipa faini ya dola 2.8 milioni (sawa na zaidi ya Tsh Sh5 bilioni) kwa kuharibu mazingira, kosa walilofanya wakati wa ujenzi wa nyumba jijini Rio Grande do Sul, Kusini mwa Brazil.

Leave a Comment