×

Janeth Magufuli Akabidhi Wheelchairs kwa Walemavu

Mke wa Rais Magufuli,  Janeth Magufuli,  akipokea shukurani za bila kushikana mikono na Mbunge wa Kilombero ( CHADEMA),  Peter Lijualikali, baada ya kumkabidhi viti mwendo (Wheelchairs) 210 kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2020. Wanaoshuhudia ni Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson na mke wa Balozi wa Tanzania nchini Israel  Joan Masima.

 

 

NAIBU Spika wa Bunge la  Tanzania,  Tulia Ackson, amemshukuru mke wa Rais Magufuli,  Janeth Magufuli,  kwa kuendelea kuwasaidia wananchi wenye uhitaji, wakiwemo watoto wenye ulemavu na wazee akitaja kitendo hicho kuwa ni cha kizalendo na chenye kutia moyo.
Jameth Magufuli akisalimiana na  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (watu wenye ulemavu)  Stella Alex Ikupa.
Tulia ametasema hayo leo wakati wa hafla fupi ya Mama Magufuli kukabidhi viti mwendo (Wheelchairs) vipatavyo 210 kwa baadhi waheshimiwa wabunge kwa ajili ya kuwagawia watoto wenye uhitaji majimboni kwao iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.
Janeth Magufuli akisalimiana na  Mama Ulega, mke wa Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Abdallah Ulega baada ya kuwakabidhi wabunge viti hivyo.
Naibu Spika  amesema kwamba katika  kuwasaidia wazee na watoto wenye ulemavu  Mama Magufuli  amekuwa mfano wa kuigwa kwa wanawake kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii ya watu wenye mahitaji.
…Akiwa na Dkt. Tulia Ackson, Stella Alex Ikupa, Mke wa Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mama Joan Masima na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sofia Mjema katika picha ya pamoja na wabunge na wawakilishi wa wabunge baada ya kuwakabidhi viti mwendo hivyo.
Mama Magufuli, ambaye ametoa msaada wa viti mwendo kwa watoto wenye ulemavu siku chache kabla ya Siku ya Wanawake Duniani, amewashukuru waheshimiwa Wabunge walioitikia mwito wake kupokea msaada huo.
Mama Magufuli akisalimiana na Dkt. Tulia Ackson, baada ya kuwakabidhi wabunge viti mwendo (Wheelchairs) 210 kwa ajili ya watoto wenye Ulemavu.

“Kama mjuavyo kila tarehe 08/03 ya kila mwaka ni Siku ya Wanawake Duniani. hivyo basi nikiwa miongoni mwa wanawake nimeguswa na kuamua kusherehekea siku hii muhimu kwetu kwa kutoa zawadi ndogo ya viti mwendo kwa waheshimiwa wabunge ili wawafikishie wanangu wenye uhitaji kwenye majimbo yao kwa urahisi zaidi, kwani wao ndio wawakilishi wa wananchi”, alisema Mama Magufuli.
PICHA NA IKULU

Leave a Comment