×

Ndinga Mpya ya Championi, Spoti Xtra Yatua Arusha

VIJANA wa siku hizi wanasema, mambo ni yente au safi ndani ya Jiji la Arusha, wenyeji hupaita R-Chuga, hii ni baada ya kuzinduliwa rasmi kwa promosheni namba moja kwa sasa Tanzania. Nazungumzia bahati nasibu ya chomoka na gari mpya aina ya Toyota FunCargo inayoendeshwa na Magazeti Bora ya michezo, Championi na Spoti Xtra mkoani Arusha.

 

 

Timu ya masoko ya Global Publishers, Kanda ya Kaskazini ikiongozwa na Chocks Chokala na MC Mashauri, jana Ijumaa ilitia timu jijini Arusha kuzindua rasmi Chomoka na Gari Mpya na kushangazwa na mapokeo makubwa ya promosheni hiyo kutoka kwa wasomaji na wa magazeti ya michezo nchini na wadau wa tasnia hiyo waliojitokeza kwa wingi kuipokea promosheni hiyo.

 

Timu ya masoko ilitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo; Stendi ndogo, Kilombero, Ngarenaro, Stendi kubwa ya mabasi ya mkoani, Uhuru Road, Soko Kuu, Sakina, Sanawari, Mbauda na Tengeru.

 

Wasomaji wa magazeti hayo walichangamkia magazeti hayo ya michezo na kujaza koponi zilizowawezesha kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kushindania gari huku wakiahidi kununua magazeti hayo zaidi na zaidi ili washiriki bahati nasibu hiyo na kujaribu bahati yao ya kushinda ndinga hiyo.

Hii ni wiki ya tatu sasa tangu Kampuni ya Global Publishers ilipozindua bahati nasibu hiyo kupitia magazeti ya Championi na Spoti Xtra, ambapo wasomaji watanufaika na ushindi wa gari mpya aina ya Toyota Funcargo.

 

Mbali na zawadi hizo, kila wiki washindi 10 wataondoka na simu janja mpya za mkononi aina ya smart kitochi zikiwa zimesheheni bando la bure na App ya Global ambayo ndani yake ina +255 Global Radio na Global TV Online.

 

JINSI YA KUSHIRIKI

Nunua Gazeti la Championi kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.

 

JINSI YA KUTUMA:

Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam. Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.

 

MASHARTI YA KUSHIRIKI:

Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.

 

Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

 

 

Leave a Comment