×

Watu wa Buza Wanataka Gari

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Global, Anthony Adam (kushoto),  akimwelekeza msomaji namna ya kushiriki bahati nasibu ya shinda gari.

WAKAZI wa Jiji la Dar es Salaam wa maeneo ya Buza na maeneo ya Kijiwe Samli wamejinasibu kununua kwa wingi magazeti ya Championi na Spoti Xtra ili washiriki kwa wingi Bahati Nasibu ya ‘Baba Lao’ inayoendeshwa na magazeti hayo ambapo mshindi wa droo kubwa ataondoka na gari mpya aina ya Tpyota FunCargo.

Adam (kushoto), akiendelea kuwaelekeza  namna ya kujaza kuponi kwa ajili ya kushiriki bahati nasibu hiyo.

Akiinadi Bahati Nasibu hiyo, Mkuu wa Idara ya Masoko ya Global Publishersl, Anthony Adam, amewahamasisha wananchi hao kununua magazeti ya Championi na Spoti Xtra ili kushiriki Bahati Nasibu hiyo kwani nafasi ya kulichukua gari hilo inaweza kwenda kwaao.

Mwanadada wa maeneo ya Buza jijini Dar es Salaam akijaza kuponi.

Amesema kuwa kadri wanavyoendelea kununua magazeti ndivyo wanazidi kujiongezea nafasi kubwa ya kuwa washindi huku akiwataka kila wanapoona gari la matangazo kujitokeza kwa wingi kukabidhi kuponi ambazo wamekwisha zijaza ama kumpelekea muuzaji wa magazeti aliye karibu nao.

Mmoja wa wasomaji wa magazeti ya Championi akikata kuponi kwa ajili ya kushiriki bahati nasibu ya ‘Baba lao’.

Akiwaelekeza namna ya kushiriki bahati nasibu hiyo, Anthony alisema;  “Unachotakiwa kufanya ni kununua magazeti hayo na kukata kuponi iliyopo ukurasa wa pili na kujaza jina lako, namba yako ya simu, anwani yako na umri wako.

Wasomaji wa Gazeti la Championi wakijadili jambo kabla ya kushiriki kujaza kuponi.

Adam ameongeza kuwa mbali na  kujishindia gari, kuna zawadi nyingine nyingi kama vile simu za mkononi za kisasa almaarufu kwa jina la Smart Kitochi na nyinginezo  ambazo zitatolewa kila mwezi kuelekea kwenye droo hiyo kubwa ya kujishindia gari.

Tabasamu la kujaza kuponi likinoga.
JINSI YA KUSHIRIKI
Nunua Gazeti la Championi kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.
Mmoja wa washiriki wa bahati nasibu akiwa amemaliza kuweka kuponi yake itakayomwezesha kuingia katika droo.

JINSI YA KUTUMA:
Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam. Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.

Msomaji wa Gazeti la Championi wa maeneo ya Kijiwe Samli jijini Dar akijaza kuponi yake.

MASHARTI YA KUSHIRIKI:
Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.

Mdau wa Gazeti la Championi akilisoma gazeti hilo baada ya kulinunua kabla ya kushiriki kujaza kuponi ya bahati nasibu .

Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

Mmoja wa washiriki wa bahati nasibu akiwa amemaliza kuweka kuponi yake itakayomwezesha kuingia katika droo.

 

NDINGA MPYA ya CHAMPIONI Yaanza Kumsaka Mmiliki Wake “WASILISHA KUPONI MAPEMA” – Afisa Masoko

Leave a Comment