×

TAKUKURU Yaokoa Bil 8 “Bado Bilioni 57, Tukaziokoa Zote” – Video

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) imeokoa zaidi ya shilingi bilioni nne, baada ya kukamilika kwa awamu ya pili ya uchunguzi wa fedha ambazo ni mali ya vyama vya ushirika ambazo hazijulikani zilipo.

Akitoa taarifa hiyo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo amesema kuwa, kuokolewa kwa fedha hizo kunafikisha shilingi bilioni 8.5 zilizookolewa tangu taasisi hiyo ipewe jukumu la kuchunguza shilingi bilioni 124 mali ya vyama vya ushirika.

Ameitaja mikoa ya kiushirika ya Njombe, Kagera, Kinondoni, Temeke na Mbeya kuwa ndiyo inayoongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha fedha ambazo hazijulikani zilipo.

Brigedia Jenerali Mbungo ametoa wito kwa watu waliojichukulia mali za vyama vya ushirika kuzirejesha haraka mahali husika. Awamu ya Tatu ya uchunguzi huo itahusisha uchunguzi wa zaidi ya shilingi bilioni 57 .

 

Leave a Comment