×

Maswali & Majibu Muhimu Kuhusu Ugonjwa wa COVID-19

MLIPUKO wa maambukizi ya Virusi vya Corona umeathiri mataifa mbalimbali duniani na bado athari zake zinaendelea kwa kasi, awali ilionekana ni jambo la taifa moja la China ambako ndiko ulikoanzia lakini sasa hali ya mambo imebadilika.

Kuna shughuli nyingi za kimichezo na burudani zimesimamishwa kutokana na virusi hivyo ambavyo vinasababishwa na Ugonjwa wa COVID-19.

 

Mfano tumeona Ligi Kuu za Ulaya zimesimamishwa, Ligi Kuu ya Bara na Zanzibar zote zimesimamishwa, hivyo kwa kiasi kikubwa Corona imechangia kuvuruga mambo mengi.

Pamoja na elimu inayoendelea kutolewa lakini kuna watu wengi pia wamekuwa wakiendelea kubaki gizani juu ya Virusi vya Corona.

Maswali makuu ni virusi hivi vinaambukizwaje kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na jinsi gani ya kujikinga kutosambaza au kuwasambazia wengine.

 

Haya hapa ni baadhi ya maswali yanayoulizwa na wengi na jinsi ambavyo wataalam mbalimbali wa afya wameyajibu au kutolea ufafanuzi:

 

JE, BARAKOA (MASK) INASAIDIA KUKINGA MAAMBUKIZI YA CORONA?

Mara baada ya kuonekana watu wa mataifa ya nje wakivaa barakoa maarufu kwa jina la mask kumekuwa na idadi kubwa ya watu wanaofuata mkumbo na kuvaa bila kuwa na elimu nzuri juu ya matumizi ya kifaa hicho.

Majibu ya wataalam yanaonyesha kuwa kuna ushahidi mdogo kuwa barakoa inasaidia kwa namna moja au nyingine.

Wataalamu wa afya wanasema kuwa usafi wa mara kwa mara wa watu kuosha mikono na kutojigusa mdomoni kunasaidia zaidi kuliko kuvaa mask ambapo pia kuna tatizo la Watanzania wengi kutovaa zile zinazoaminika kuwa na ubora mzuri wa kuzuia majimaji ikitokea mtu wa pembeni amepiga chafya.

JE, VIRUSI VYA CORONA VINAWEZA KUNASA KATIKA VITASA? KAMA NDIYO VINAKAA HAPO KWA MUDA GANI? KAMA MTU ANA MAAMBUKIZI NA AKIKOHOA KATIKA MKONO WAKE NA BAADAYE KUSHIKA KITU, JE KITU HICHO KINAWEZA KUPATA MAAMBUKIZI?

 

Vitasa vya mlango ni mfano mzuri zaidi kuwa kuna hatari kubwa ya kupata maambukizi kama mtu mwenye Corona akishika mlango wakati alikoholea mkono wake.

Wataalamu wanadhani kuwa Virusi vya Corona vinaweza kukaa kwa muda wa siku kadhaa.

Hivyo, namna nzuri ya kukabiliana na jambo hili ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi ni kunawa mikono mara kwa mara.

JE, NIKIKUTANA KINGONO NAWEZA KUPATA MAAMBUKIZI?

Haijawa wazi kama watu wakikutana kimwili wanakuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya Corona.

Kwa sasa ni kukohoa na kupiga chafya ndiyo mambo yanayotajwa kuwa hatari katika maambukizi.

 

KUNA UTOFAUTI GANI KATI YA CORONA NA MAFUA?

Dalili za maambukizi ya Virusi vya Corona na mafua yanafanana kwa kiasi kikubwa, hivyo inafanya tiba kuwa ngumu bila kupimwa.

Dalili za Virusi vya Corona vinaweza kuanza kwa homa na kukohoa.

Mafua mara nyingi huwa yana dalili nyingine kama koo kuwasha, huku watu wenye Virusi vya Corona huwa wanaweza kuishiwa pumzi kidogo.

 

JE, VIRUSI VYA CORONA VINAAMBUKIZA ZAIDI YA MAFUA?

Ni mapema mno kuweza kulinganisha lakini virusi vyote vinaambukiza.

Kwa wastani Virusi vya Corona vinaweza kuambukiza watu wawili au watatu huku virusi vya mafua huwa ni kama vinatoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine.

Ingawa maambukizi yote ya mafua na Corona huwa yanasambaa kwa haraka.

 

JE, MTU ANAWEZA KUPATA VIRUSI VYA CORONA KWA KULA CHAKULA KILICHOANDALIWA NA MTU MWENYE MAAMBUKIZI YA CORONA?

Mtu mwenye maambukizi ya Corona kama amepika bila kuzingatia usafi basi moja kwa moja anaweza kumuambukiza mtu mwingine Virusi vya Corona.

Virusi vya Corona vinaweza kusambaa kwa matone ya kikohozi yaliyo kwenye mkono.

Kuosha mikono kabla ya kushika na kula chakula ndiyo ushauri unaotakiwa kuuzingatia.

 

NICHUKUE TAHADHARI GANI?

Kwa watu wanaoishi Italia na maelfu ambao wanasafiri maeneo mbalimbali duniani, wako kwenye hatari ya maambukizi zaidi.

Maambukizi yanasambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, kwa njia ya matone ya kikohozi.

Ni muhimu kwa watu kuzingatia kuosha mikono mara kwa mara kwa maji yanayotiririka na sabuni au dawa ya kuosha mikono (sanitizer).

Ni vyema kujizuia kutokuwa karibu na mtu anayekohoa au mwenye homa.

Mtu yeyote anayedhani kuwa amepata maambukizi ya Corona ni bora kumpigia simu daktari au katika mamlaka husika, pia anaweza kufika hospitalini haraka kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

 

JINSI GANI YA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA?

Baadhi ya mataifa yamepiga marufuku kwa watu kukutana katika mikusanyiko, ndivyo ambavyo Serikali ya Tanzania pia imefanya hivyo, ikiwemo kufunga shule ngazi zote kwa muda wa mwezi mzima.

 

INAWEZEKANA UGONJWA HUU KUPATA CHANJO?

Kwa sasa hakuna chanjo ya kujikinga na Virusi vya Corona, ingawa wanasayansi bado wanapambana kutengeneza chanjo ya aina hiyo.

 

JE, MABADILIKO YA TABIA NCHI YANACHANGIA ATHARI ZINAZOJITOKEA KATIKA VIRUSI VYA CORONA?

Haijawekwa wazi kama mabadiliko ya hali ya hewa yanachangia maambukizi. Baadhi ya virusi kama vya mafua huwa vinakuja mara nyingi katika wakati wa baridi kali.

 

JE, MTU ALIYEUGUA UGONJWA WA CORONA ANAWEZA KUPATA MAAMBUKIZI TENA?

Virusi hivi vipya vya Corona, vinaweza kusababisha mtu uugue na wengi ni watu wenye shida ya mapafu, lakini virusi hivi vipya hakuna ambaye ana kinga dhidi yake.

Hivyo haijalishi kama uliugua mwanzo au la, aidha Shirika la Afya Duniani limesema kuwa kabla ya miezi 18 kupita chanjo ya Corona

Leave a Comment