×

Morrison: Nafunga Kwanza Kisha Shoo

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mghana Bernard Morrison, amefunguka kuwa mpango ambao anakuja nao kwa sasa ni kuhakikisha timu hiyo inafunga mabao mengi kisha ndiyo anaanza mpira wa kuwafurahisha mashabiki.

 

Mghana huyo amesema kwamba licha ya kwamba ana vitu vingi vya kiuchezaji ambavyo hajavionesha lakini kwa  asa anafikiria kufunga zaidi kisha ndiyo awaburudishe mashabiki kwa staili zake ikiwemo

kupanda mpira.

 

Tangu asajiliwe na Yanga katika usajili wa dirisha dogo Januari, mwaka huu, Morrison amefanikiwa kufunga mabao matatu katika kikosi hicho.

 

Morrison amesema kwamba bado ana staili nyingi ambazo hajazionyesha kwa mashabiki wake lakini kwa sasa anahakikisha kwamba anapambana kufunga mabao mengi zaidi.

 

“Nilipokuwa Afrika Kusini ndiko nilijifunza staili na mitindo mingi ya kiuchezaji ambayo mingine bado sijaionyesha kwa mashabiki hapa.

 

“Lakini hilo ni jambo moja lakini kwanza tunataka kufunga mabao mengi kwenye mechi zetu kisha mengine yatafuata. Najua wanapenda ninavyofanya na ndiyo maana wanakuja uwanjani kufurahi lakini nitafanya zaidi baada ya kufunga mabao mengi,” alisema Morrison.

Said Ally, Dar es Salaam

Leave a Comment