×

Yanga Ilivyoizidi Ujanja Simba kwa Morrison

MASHABIKI wa Yanga hivi sasa watakuwa wanapumua, ni baada ya wadhamini wao GSM kufanikisha jaribio la kiungo mshambuliaji Mghana Bernard Morrison la kwenda kusaini Simba, iliyokuwa inamuwania vikali nyota huyo.

 

Mghana huyo aliyecheza mechi 13 akipiga asisti tatu huku akifunga mabao manne kwenye michuano yote, alijiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu wa Ligi Kuu Bara, akisaini mkataba wa miezi sita. Lakini juzi aliongeza mkataba mwingine wa mwaka mmoja na nusu wakati Simba wakiwa mbioni kumsajili.

 

Yanga walifanikiwa kumsajili kiungo huyo akiwa katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa kwenda Simba, baada ya kuvutiwa na kiwango chake ambacho amekionyesha katika michezo aliyoichezea huku akiwafunga katika mchezo wa jadi uliopigwa hivi karibuni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Championi Jumatatu linakuletea mahojiano maalum yaliyofanywa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela ambaye ameelezea mchezo mzima ulivyokuwa jinsi walivyofanikisha mipango hiyo ya kuikimbia Simba.

 

KIGOGO TFF AISHTUA YANGA

“Tulikuwa tunahisi kitu kwa Simba juu ya kumtaka Morrison, lakini tunashukuru mmoja wa maofisa wa TFF ndiye aliyetutonya kuwa tuwe makini na Morrison, kama mkataba wake unamalizika basi haraka tumuongezee.

 

“Alitutahadharisha mapema tu, na hiyo ni baada ya Simba kwenda TFF kuulizia mkataba wake na kuambiwa kuwa unamalizika mwishoni mwa msimu, hivyo ni mchezaji huru anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine itakayomhitaji.

 

“Baada ya kushtukia hilo, haraka tukafanya kikao cha viongozi kwa kuishirikisha kamati ya usajili yenye wajumbe wazito akiwemo injinia Hersi Said kutoka GSM na kufikia makuba liano mazuri ya kuha kikisha tunapa mbana ili kumbakisha.

“Kama siyo kigogo wa TFF kututonya, basi Yanga tungemkosa Morrison na hiyo ni kutokana na mimi kuwa na watu pale shirikisho, kama unavyofahamu niliwahi kufanya kazi pale.

 

SIMBA WAMFUATA MORRISON, AWAPELEKA KWA MENEJA WAKE SAUZ

“Baada ya viongozi wa Simba kwenda TFF, haraka wakamfuata meneja wa Morrison aliyepo nchini Afrika Kusini na haraka wakaanza mazu ngumzo kwa ajili ya kufanikisha usajili huo.

“Ilikuwa rahisi kwa meneja wa Morrison kukubali kumuachia kwenda Simba kutokana na yeye kutojua upinzani uliopo kati ya timu hizi mbili za Simba na Yanga.

 

“Na Simba ilimfuata meneja wa Morrison Afrika Kusini baada ya mchezaji mwenyewe kuwaambia kuwa yeye hawezi kuzungumzia suala lolote la usajili na kama wanamtaka kweli, basi wamfuate meneja wake huyo.

 

NGOMA NGUMU, MWAKALEBELA AMPIGIA SIMU MMILIKI WA GSM

“Baada ya kuona watani wetu Simba wapo ‘siriazi’ na hawatanii, haraka nikampigia simu mmiliki wa GSM, Gharib na kumuelezea sakata hilo na yeye haraka akampigia simu Hersi na kufanikisha dili hilo.

“Kikubwa Gharib alitutoa hofu na kuahidi kutoa kiasi cha pesa ambacho Morrison anakitaka ambacho kilikuwa kikubwa kwa kweli, lakini nashukuru alifanikisha hilo.

 

KUMBE SIMBA ILIANDAA MKATABA WA MORRISON

“Wenyewe Simba walikuwa wanafanya siri, lakini sisi tulikuwa tunajua kila kitu kilichokuwa kinaendelea na walichokuwa wanakifanya, tunajua wanataka vita na sisi, hivyo wajiandae kuwa tutapiga pigo moja kubwa pale Simba,” alisema Mwakalebela.

 

HUYU HAPA MORRISON, AFUNGUKA

“Nilikuwa nashangazwa na habari kwamba ninajiunga na Simba ilihali nilikuwa naitumikia Yanga, ninachokijua mimi ni mali ya Yanga na nitaendelea kuitumikia timu yangu hii pendwa.

“Kuhusu kutakiwa na Simba ni vitu ambavyo vipo ukizingatia mimi ni mchezaji hata nilipokuwa nje ya Tanzania kuna timu zilikuwa zinanihitaji ila mwisho wa siku nikajiunga na Yanga.

 

“Nawapenda mashabiki wa Yanga wamekuwa wakionyesha tabia za kipekee kwa kujitokeza uwanjani na kufurahi pamoja nasi, nami nitaendelea kupambana ndani ya Yanga,” alisema Morrison.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave a Comment