Serikali imepokea msaada wenye thamani ya Sh Bilioni 3.2 kutoka taasisi mbalimbali jijin kwa ajili ya kupambana na maamumbizi ya ugonjwa wa corona. Taasisi hizo zikabidhi msaada huo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambaye alipokea kwa niaba ya waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Kampuni ya simu, Vodacom Tanzania ilikabidhi kiasi cha Sh bilioni 2 wakati taasisi ya Letshego (Faidika) ilikabidhi msaada wenye thamani ya Sh milioni 33 huku Yapı Merkezi ikitoa msaada wenye thamani ya Sh milioni 200.
Katika orodha hiyo pia ni benki ya NBC iliyokabidhi sh milioni 80 , wakati Shirika la Reli Tanzania lilikabidhi Sh Milioni 65 na Rotary Bahari ilikabidhi msaada wenye thamani ya Sh milioni 15.
Kampuni ya Songas Limited nayo ilikabidhi msaada Sh milioni 100 wakati kampuni ya Bima ya Sanlam ilitoa msaada wa Sh milioni 172.5, Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya fedha Tanzania (FSDT) ikikabidhi Sh million 225 na Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri ikiabidhi msaada wa Sh milioni 10.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Lestshego (Faidika) Andrew Tarimo amesema kuwa wameguswa sana na vita dhidi ya kutokomeza ugonjwa wa corona na kuamua kutoa kiasi hicho cha fedha ili kusaidia Watanzania.


