
MBUNGE wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo, amekutana na wakuu wa shule za msingi na sekondari na maafisa elimu wa kata zote za halmashauri ya Buchosa kwa lengo la kujadili namna ya kuinua kiwango cha elimu katika halmashauri hiyo.
Shigongo amefanya kikao hicho kinachotokana na matokeo mabovu ambayo yalisababisha kushika nafasi za mwisho katika mitihani ya taifa ya darasa la saba mwaka jana.
Amesema katika vitu ambavyo vinamuumiza Buchosa ni suala la elimu kwani anaamini kuna watoto wengi sana wenye akili katika maeneo hayo ya vijijini lakini mazingira duni ya kielimu yamekuwa yakiwafanya kuonekana hawana akili na kufeli mitihani yao.
Aidha,amesisitiza kuwa ataanza kutoa motisha kwa walimu ambao watafanya vizuri katika masomo yao kwa kufaulisha wanafunzi, hivyo ni vyema walimu wakajituma kufundisha kwa bidii ili kuinua kiwango cha ufaulu wa mitihani kwa watoto Buchosa.