×

Video: Selasini Ajiondoa Chadema, Atimkia NCCR-Mageuzi

MBUNGE wa Rombo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Selasini ametangaza kuachana na chama hicho na kurejea kwenye chama chake cha awali cha NCCR Mageuzi mara tu baada ya bunge litakapovunjwa Juni 30, 2020.

 

Selasini ametangaza uamuzi huo leo Aprili 28, 2020 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dodoma na kuiomba NCCR impe nafasi ya kugombea ubunge kwenye jimbo lake la Rombo.

 

Awali, kulikuwa na taarifa zinazoeleza kuwa Mbunge huyo ameonesha kusikitishwa baada ya kuondolewa bila kupewa taarifa kwenye ‘Group la WhatsApp’ la Wabunge wa CHADEMA. Imeelezwa kuwa katika ‘group’ hilo yumo pia Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe.

 

Leave a Comment