×

Jeneza Lililozua Kizaazaa Arusha, Mmiliki Afungukia Utapeli – Video

Muda mfupi baada ya tukio lisilo la kawaida kuzua kizaazaa mkoani Arusha baada ya jeneza lenye mkungu wa ndizi ndani yake kutelekezwa katika shamba lililopo Mtaa wa Bondeni, Kata ya Endaseni wilayani Arumeru mkoani Arusha, mmiliki wa shamba lilipokutwa jeneza hilo, amefafanua kwa kina.

 

Akizungumza na mwandishi wetu, Abraham Palangyo ambaye ndiye mmiliki halali wa shamba hilo, amesema kumekuwepo na mgogoro kati ya familia hiyo na mwanamke mmoja anayedai kuuziwa eneo hilo na madalali ambao hawafahamiki kwa kiasi cha shilingi milioni 30.

 

Ameongeza kuwa, waliamua kulipeleka suala hilo mahakamani, baada ya mwanamke huyo kuanza kufanya shughuli mbalimbali ndani ya eneo hilo, wakati familia ikiwa haijui wala haihusiki na mauziano hayo  yaliyofanyika, ambayo yanaonesha sura ya utapeli ambapo baada ya mahakama kujiridhisha kuwa mmiliki halali ni Palangyo, siku kadhaa baadaye ndipo jeneza hilo lilipokutwa katika eneo hilo.

 

Tazama video kujionea zaidi alichokisema mmiliki huyo huku akiungwa mkono na mwanaye na majirani.

 

Leave a Comment