KLABU ya Arsenal ipo tayari kumuachia nahodha wake Pierre-Emerick Aubameyang kwa kiasi cha pauni 30m kuliko kumuacha kuondoka kama mchezaji huru.Aubam-eyang mkataba wake ndani ya Arsenal unatarajiwa kumalizika Juni, 2021 na amekuwa akishindikiza kuondoka ndani ya klabu hiyo.
Klabu tofauti zimetajwa kuwania staa huyo kama Inter Milan, Barcelona, Manchester United huko klabu hizo zikitajiwa kiwango cha juu cha fedha.
Aubameyang alijiunga na Arsenal msimu wa mwaka 2017/18 akitokea katika klabu ya Borrusia Dortmund ya Ujerumani ambako alifanya vizuri hasa katika upachikaji wa mabao.
Hata hivyo, Arsenal imejaribu kufanya mazun-gumzo naye mara kadhaa kwa ajili ya kumuongeza mkataba mpya, lakini imeonekana kushindikana.
Arsenal kwa sasa inaonekana kama imechoka na ipo tayari kumuachia kwa kiasi cha pauni 30m kwa klabu ambayo inamuhitaji.
