MMILIKI wa mabasi ya Kirumo Charo na Katibu Mkuu wa chama cha wamiliki wa mabasi TABOA, Ndg. Enea Mrutu ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Shighatini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro, amefariki dunia baada ya kubanwa kifua ghafla katika Zahanati ya Mwirange Mwanga.
