×

TPDC Yazindua Eneo la Mradi wa Maghala Mafuta na Gesi

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi alikabidhi mfano wa hundi kwa malipo ya fidia kwa wananchi waliotoa maeneo yao kupisha ujenzi wa mradi huo.

SIKU chache baada ya TPDC kurejea rasmi katika biashara ya MAFUTA pamoja na kufungua vituo vyake vya mafuta vilivyoko sehemu mbalimbali nchini, leo tarehe Juni 12, 2020 TPDC imezindua eneo la mradi wa kujenga maghala ya kuhifadhia mafuta na gesi katika eneo la Zuzu Mkoani Dodoma.

 

Uzinduzi huo umefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi ambapo alikabidhi mfano wa hundi ya malipo ya fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa mradi pamoja na kufungua rasmi ujenzi wa mradi huo.

 

Katambi alisema kwamba “kujengwa na kukamilika kwa mradi huu kutatoa fursa mbalimbali zikiwemo ajira kwa wananchi wa Kata ya Zuzu”.

 

Ndugu Juma Boniphace moja Kati ya wananchi ambao wametoa maeneo yao kupisha ujenzi wa Mradi, akitoa Shukrani kwa niaba ya wananchi wenzie.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio alisema kwamba, mradi wa ujenzi wa Maghala ya kuhifadhia mafuta na gesi utakapokamilika utapunguza gharama za usafirishaji ambapo kwa sasa nishati hiyo ya mafuta inafuatwa Dar Es Salaam hivyo kusababisha nishati hiyo kuwa ya Bei ya juu na kutopatikana maeneo ya vijijini.

 

Ujenzi wa Maghala hayo kutawezesha nishati hiyo kupatatikana kwa bei nafuu hasa katika maeneo ya vijijini.

Mkurugenzi Mtendaji a TPDC (mwenye fulana) akionesha kwa Mkuu wa Wilaya Mhe. Patrobas Katambi mfano wa hundi kuonesha malipo yaoiyolipwa na TPDC.

Kwa upande mwjngine Dkt. Mataragio aliwatoa hofu wafanyabiashara wa mafuta kutoka kampuni binafsi ya kwamba kuingia kwa Serikali katika biashara ya mafuta hauna lengo la kuuondoa wafanyabiashara hao bali TPDC inaingia kwa ushindani. Baada ya uzinduzi huu, maghala mengine yatajengwa Tanga pamoja na Mwanza.

TUMEAMUA NA TUNATEKELEZA, TPDC TUNAWEZESHAA

Leave a Comment