×

Global Habari June 14: Viongozi CCM Watakiwa Kutenda Haki Uchaguzi Mkuu

Mlezi wa chama cha mapinduzi CCM kanda ya kati na waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda amewata viongozi wa kamati za siasa za chama hicho Mkoani Dodoma, kutenda haki na kuepuka rushwa katika kupitisha majina ya wanaogombea nafasi za uchaguzi mkuu mwaka huu Pinda ametoa maagizo hayo jijini Dodoma wakati akikamilisha ziara yake ya siku nne katika wilaya zote za Mkoa huo huku akisisitiza uadilifu ndani ya Chama hicho

 

Aidha Mizengo Pinda ametumia fursa hiyo kwa kuwataka viongozi ndani ya chama hicho kushirikiana na kuachana na tabia ya malumbano kama anavyobainisha hapa Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka huu, huku ukihusisha nafazi za uongozi katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Urais,ubunge na udiwani

Leave a Comment