
ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, ametoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha, Iddy Kimanta, kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuapishwa jana Juni 22, 2020, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Baada ya uapisho huo Gambo aliandika ujumbe ufuatao:
Hongera sana Mzee wangu Iddy Kimanta Kwa kuteuliwa na kuapishwa Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Nakutakia kila la heri na Mungu akakusimamie kwenye kazi zako. Rais Magufuli kafanya mambo mengi na makubwa Arusha.