
MWEKEZAJI wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kuanzia sasa akitokea Dubai tayari kwa baada ya kucheza mechi 32 huku wapinzani wao, Yanga wakiwa na pointi 60 hadi sasa.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe, amefunguka kuwa, wameandaa ‘surprise’ kuwapatia ‘surprise’ wachezaji wa Simba baada ya ubingwa walioutwaa wa Ligi Kuu Bara.

Simba tayari imeshafanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu baada ya kufikisha pointi 79 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote ya ligi kwa wachezaji wao mara baada ya mwekezaji wao, Mo Dewji atakaporejea kutoka Dubai ili kuweza kushangilia pamoja ubingwa pamoja na wachezaji na benchi la ufundi.
“Kiongozi wetu Mo kwa sasa hayupo hapa nchini, yupo nje ya nchi, nchini Dubai na anatarajia kurejea wakati wowote kuanzia sasa ambapo akifika ndipo atakuja kushangilia ubingwa pamoja na wachezaji akiwa kama kiongozi wetu kwa ajili ya kuwapatia zawadi.
“Tumepanga kuwapa zawadi ambayo itakuwa ni ‘surprise’ kama ilivyokuwa mwaka jana walipopewa pikipiki, safari hii kuna kitu watapewa, hivyo hatuwezi kuweka wazi ni zawadi gani kwani zawadi ukiiweka wazi inakuwa siyo ‘surprise’ tena,” alisema Kashembe.
STORI: Khadija Mngwai,Dar es Salaam