×

Tshishimbi Aiwahi Simba FA Cup

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael amefunguka kuwa ana uhakika nahodha wa timu hiyo, Papy Tshishimbi, raia wa DR Congo, atakuwa sawa kabla ya mchezo wao dhidi ya Simba katika Kombe FA.

 

Simba imetinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA baada ya juzi Jumatano kufanikiwa kuwafunga Azam mabao 2-0 ambapo sasa wataivaa Yanga, Julai 12, mwaka huu.Tshishimbi ambaye alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya goti yaliyosababisha kuwa nje kwa wiki mbili, tayari ameanza mazoezi mapesi na kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mechi zijazo ikiwemo ya Simba.

 

Eymael amesema kuwa anaamini nahodha huyo atauwahi mchezo wao dhidi ya Simba kutokana na kuanza mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa madaktari wa timu hiyo.

“Tshishimbi anaendelea vizuri na ameanza mazoezi mepesi chini ya uangalizi maalum wa madaktari wa timu, matarajio yangu atakuwa sawa hivi karibuni.

 

“Nadhani nitamkosa katika mechi mbili za ligi kuanzia dhidi ya Kagera lakini kuhusu mechi yetu dhidi ya Simba atakuwa tayari ameshakuwa sawa kwa kuwa atakuwa na muda wa kutosha kufanya mazoezi kabla ya mchezo huo,” alisema Eymael.Naye, Daktari wa Yanga, Shecky Mngazija alipoulizwa juu ya mchezaji huyo alisema: “Anaendelea vyema na leo (jana) ameanza mazoezi pepesi, akiwa sawa ndiyo atajiunga na wachezaji wenzake.”

STORI: BRAHIM MUSSA NA KHADIJA MNGWAI,

Leave a Comment