×

Kaseke, Makame Wazua Hofu ya Ushirikina

WACHEZAJI wawili wa Yanga, viungo Deus Kaseke na Abdulaziz Makame, walisababisha minong’ono na kuhisiwa kuwa wanafanya ushirikina baada ya wote wawili kupiga mipira juu wakiwa nje ya eneo la kuchezea na kisha mipira hiyo ikaingia uwanjani.

 

Tukio hilo lisilo la kawaida lilitokea wakati wachezaji wa Yanga wakielekea uwanjani kupasha misuli joto kwa ajili ya mtanange wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Simba ilikuwa timu ya kwanza kuingia uwanjani kupasha misuli majira ya saa 10, ikafuatiwa na Yanga. Kwa upande wa Yanga, beki Juma Abdul na kipa Metacha Mnata ndio waliokuwa wa kwanza kuingia uwanjani wakifuatiwa na wachezaji wengine.

 

Wakiwa wanaingia, kituko kilitokea baada ya Kaseke na Makame kusimama nje ya uwanja (eneo la kuchezea) na kupiga mipira juu kuelekea uwanjani.

 

Kitendo hicho kilisababisha kelele kutoka kwa mashabiki wa Simba waliohisi kwamba huenda ni cha kishirikina, yaani ‘maelekezo kutoka kwa mganga’, hata hivyo hakuna anayeweza kuwashutumu kwa kuwa hakuna mwenye uhakika juu ya hilo zaidi ya kuhisi tu.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave a Comment