×

Makonda Kuwania Ubunge Kigamboni

MKUU  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo Julai 15, 2020,  amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya ubunge Jimbo la Kigamboni kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Hadi Bunge linavunjwa Juni 16, 2020, Jimbo la Kigamboni lilikuwa chini ya Dkt. Faustine Ndugulile aliyeondolewa kwenye nafasi ya Naibu Waziri wa Afya

Katika uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Februari 11, 2020, Makonda alimuomba ruhusa Rais John Magufuli ili  aweze kuifanya Wilaya ya Kigamboni kufanana na kitongoji cha  Manhattan kilichopo jijini New York, Marekani.

Aidha, Julai 12, 2020,  alitoa msaada wa magari na vifaa tiba kwa hospitali ya Wilaya ya Kigamboni na kusema amefanikiwa kupata wadau watakaompatia vifaa kwa ajili ya watoto njiti na muda wowote vitakabidhiwa kwa hospital hiyo

ONA MAPOKEZI YA DKT MWINYI AKIWASILI Z’BAR | AFANYA DUA KUMUOMBEA HAYATI ABEID KARUME

Leave a Comment