×

Azam FC Kushusha Vifaa vya Kimataifa

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utafanya usajili wa wachezaji wa kimataifa wenye viwango vizuri ili kuirudisha timu hiyo kwenye ubora ikiwa ni pamoja na kugombea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao na kufuzu kushiriki michuano ya kimataifa.

 

Azam FC msimu huu imeshindwa kufanya vizuri baada ya kushindwa kutwaa kombe lolote huku pia ikishindwa kufuzu kushiriki michuano ya kimataifa kwa msimu ujao.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Azam FC, Thabit Zacharia, alisema kuwa uongozi wa timu hiyo, umepanga kufanya usajili wa maana wa wachezaji wa kimataifa ili kuirudisha Azam FC katika ubora wa awali ikiwa ni pamoja na kugombea ubingwa mwakani na kufuzu michuano ya kimataifa.

 

“Kocha ameshajulishwa juu ya kufanya usajili wa wachezaji atakaowahitaji, uongozi wa Azam unahitaji kuiona timu yetu msimu ujao ikiwa tofauti na hii ya sasa ambayo imemaliza ligi ikiwa nje ya mipango yake.

 

“Sasa mipango ya uongozi ni kuona Azam inapambania ubingwa kwa msimu ujao pamoja na kufuzu michuano ya kimataifa na ndiyo maana ili yafikiwe malengo hayo kutakuwa na usajili wa wachezaji wa kimataifa na wa maana,” alisema kiongozi huyo.

Ibrahim Mussa na Abdulghafal Ally

Leave a Comment