×

Samatta Aomba Radhi Kuvaa Barakoa – Video

Mchezaji wa Klabu ya Aston Villa na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Mbwana Ali Samatta amewaomba radhi Watanzania kwa kuingia kwenye ukumbi wa mkutano na wanahabari huku akiwa amevaa Barakoa kujikinga na Corona wakati watu wengine wote wakiwa hawajavaa Barakoa. 

 

Samatta amesema hayo leo Jumatano, Agosti 5, 2020, jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa SAMAKIBA msimu wa tatu.

 

“Kwanza niombe radhi kwa kuingia nikiwa nimevaa barakoa, huku kwetu ni tofauti na nchi za wenzetu, tukio hili ni kubwa linahusisha umati wa watu na viongozi wa timu yangu wanafuatilia, hivyo wakiona sichukui hatua hata moja ya kujikinga na corona italeta mashaka. Kwa hiyo nimefanya hivi kulingana na sheria za timu yangu, mnisamehe sana ndugu zangu.

 

“SamaKiba ina lengo moja tu la kuwasaidia watu wenye uhitaji, niwaombe watu maarufu nchini kusaidia kupost mchezo wetu unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi hii, Agosti 8, 2020. Timu yangu imejiandaa vizuri na tunaamini tutashinda tena kwa mara ya tatu mfurulizo.

 

Kuna watu wanaogopa kupost wakihisi mimi na Alikiba tutafaidika kumbe sivyo hii ni kwa ajili ya kusaidia jamii, naomba tusiangalie tofauti zetu ukahis wewe una bifu na Samatta ukakataa kutusapoti au una bifu na Alikiba ukakataa kusapoti naomba tushirikiane wote,” amesema Samatta.

Leave a Comment