×

Malkia Kareen: Ni Mwendo wa Kusaka Pesa

Sexlady kunako anga la muziki wa Bongo Fleva Karen Habash ”Malkia Karen” amesema kuwa  hakuna muda wa kulala ni muda wa kusaka pesa.

 

Akizungumza na  Risasi Malkia Karen amesema kuwa ameshukuru sana Serikali kuruhusu shoo zifanyikie kwa sababu hali za wasanii zilikuwa mbaya kiasi kwamba wengine walishindwa hata kulipa kodi za nyumba.

 

‘ Naishukuru sana Serikali ya Tanzania kuruhusu shoo ziendele maana siyo masihara hali zetu zilikuwa ni mbaya, kwa sasa hivi hakuna kuremba tena ni mwendo wa kusaka pesa.”alisema Malkia Kareen.

Stori: Khadija Bakari

Leave a Comment