×

Putin Atangaza Chanjo ya Kwanza ya Corona Duniani

RAIS Vladimir Putin wa Russia ametangaza leo kuwa nchi yake imetengeneza chanjo ya kwanza kabisa dhidi ya virusi vya corona inayotoa kinga ya kudumu.

 

Amesema kuwa tayari binti yake mmoja amepewa chanjo hiyo inayozuia kuambukizwa virusi vya corona na maradhi ya COVID-19.

 

Televisheni ya Russia Today imeripoti kuwa amesema katika mazungumzo yake ya mawaziri wa serikali yake kwamba: “Mapema leo na kwa mara ya kwanza kabisa duniani, tumesajili chanjo ya kwanza dhidi ya virusi vya corona nchini Russia.”

 

Ameongeza kwamba chanjo hiyo imevuka awamu zote za majaribio. Wiki kadhaa zilizopita Naibu Waziri wa Afya wa Russia, Olek Grenev,  alikuwa ametangaza kuwa chanjo hiyo imeingia katika majaribio ya mwisho.

 

Vilevile mwezi uliopita afisa mmoja wa ngazi za juu wa Wizara ya Afya ya Russia alitangaza kuwa inatarajiwa kwamba chanjo ya virusi vya corona itaanza kuzalishwa kwa wingi nchini humo mwezi Septemba mwaka huu.

Credit: Parstoday.

 

Leave a Comment